EDEN HAZARD AONA MWEZI CHELSEA IKIUA 4-1 ...Fabregas weka mbali na watoto ...Sothampton nayo yapiga 4-2 ...Liverpool yabandwa
Hatimaye Eden Hazard amefunga mara mbili wakati Chelsea ikiiadhibu Bournemouth 4-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Hii ni mara ya kwanza kwa Hazard kufunga katika Premier League msimu huu uanze.
Pedro Rodriguez alikuwa wa kwanza kuifungia Chelsea dakika ya 5, Hazard akafunga goli la pili dakika ya 34 huku Willian akitupia bao la tatu dakika ya 71 kabla Hazard hajafunga kwa mara nyingine dakika ya 90 kuhitimisha karamu ya Chelsea iliyokuwa ugenini. Bao pekee la Bournemouth lilifungwa na Tommy Elphick dakika ya 36.
Kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas aling'ara sana kwa nyendo na pasi zake za uhakika zilizochangia magoli matu.
Matokeo ya mechi zote za Premier League zilizochezwa Jumamosi ni:
Manchester City 4 - 0 Stoke City
AFC Bournemouth 1 - 4 Chelsea
Aston Villa 2 - 4 Southampton
Liverpool 2 - 2 Newcastle United
Bournemouth (4-4-2): Boruc 6; Francis 7, Elphick 7, Cook 5, Daniels 5.5; Stanislas 6.5 (Ritchie 78), Surman 6.5, Gosling 6, Pugh 6.5; Grabban 5.5 (Afobe 63, 6), King 6.5 (Wilson 63, 6)
Chelsea (4-2-3-1): Begovic 5; Azpilicueta 5.5, Mikel 6, Ivanovic 6, Baba 5; Matic 7, Fabregas 9; Pedro 7, Willian 7.5 (Loftus-Cheek 83), Hazard 8; Costa 6
Eden Hazard amefunga kwa mara ya kwanza katika Premier League msimu huu
Hazard akifunga kwa shuti la mita 20 dakika ya 35
Hazard akipongezwa
Comments
Post a Comment