EDEN HAZARD AMEFANYA MAAMUZI JUU YA HATMA YAKE CHELSEA


EDEN HAZARD AMEFANYA MAAMUZI JUU YA HATMA YAKE CHELSEA

Eden Hazard's future

Eden Hazard amemwambia kocha anayekuja Chelsea Antonio Conte kwamba atasalia kwenye kikosi hicho licha ya kuwepo kwa taarifa zilizosambaa kwenye vyombo vya habari kwamba ataihama klabu hiyo.

Mbeligiji huyo ambaye alishinda tuzo ya mchezaji bora wa Premier League amekuwa hayuko kwenye kiwango kizuri msimu huu huku akiwa bado hajafungia Chelsea goli hata moja kwenye meechi za EPL.

Hazard amekuwa akihusishwa kuhama Stamford Bridge  huku vilabu vya Real Madrid na Paris St-Germain kwa pamoja vikihusishwa kuitaka saini ya nyota huyo.

Laikini kwa mujibu wa gazeti la The Times, mshabuliaji huyo mwenye miaka 25 ambaye anamkataba wa miaka minne na The Blues, amemwambia boss wake ajaye kwamba anahitaji kuendelea kubaki Stamford Bridge kuliko kuondoka.

Kocha huyo wa kitaliano amefurahishwa na taarifa za Hazard kutaka kubaki na yuko tayari kumpa nafasi ya kuonesha makali yake kwenye kikosi atakachokiongoza.

Chelsea ambao ni mabingwa watetezi wa taji la EPL wapo nafasi ya 10 huku wakiwa wamesaliwa na michezo mitano, pointi 16 nyuma ya timu za top four.



Comments