DEMU WA LIONEL MESSI KWA WIVU USIPIME



DEMU WA LIONEL MESSI KWA WIVU USIPIME

SHABIKI wa Barcelona, Curvy Suzy Cortez, ambaye ni mshindi wa shindano la urembo la Miss BumBum Brazil 2015, amedai kuzuiwa kuingia katika ukurasa wa Instagram wa Lionel Messi kutokana na wivu wa mpenzi wa staa huyo, Antonella Roccuzzo.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, mrembo huyo mwenye miaka 25, amekuwa akitupia picha kibao zenye ushawishi wa mapenzi kwenye ukurasa huo wa Instagram zinazotafsiriwa kuwa na lengo la 'kumtega' Messi.

Katika moja ya picha hizo, mwanamitindo huyo Mbrazili anaonekana amepozi na jezi ya Barcelona, huku akiwa amevaa chupi nyembamba iliyogawa makalio yake, akimpongeza Messi kwa kushinda tuzo yake ya tano ya mwanasoka bora wa dunia.

Picha nyingine, inamwonyesha Suzy akiwa amepozi 'nusu-uchi' huku akiwa amevaa kofia ya Barcelona na kuweka juu ya bega lake viatu vya soka vya Messi vyenye nembo ya Adidas.

Kwa mara nyingine tena, Suzy alionekana pichani akionyesha maumbile yake, akiwa amevaa jezi maarufu namba 10, akivinjari kwenye pwani ya Ureno.

Mrembo huyo licha ya kumshambulia Antonella kwamba ana wivu na amechukua hatua kali kwa picha zake zenye mvuto wa mahaba, alijitetea kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa Barcelona na hakuna cha zaidi.

Suzy ambaye anajulikana nyumbani kwao Brazil kwa sifa yake ya kupenda "kutoka" na wanasoka alisema: "Nilishtushwa wakati nilipobaini hili. Kama ningaliweza, ningalimwambia asiwe na wasiwasi juu yangu, mimi ni shabiki tu. Nilishangaa kwamba yeye mwenyewe hana uhakika zaidi.

"Nadhani inaweza kuwa ni kwa sababu tu ana wivu. Ni mbaya sana kwa sababu mimi ni shabiki tu wa soka na shabiki mkubwa wa Barcelona."

Messi na Antonella ni wapenzi wa tangu utotoni na walijuana wakati wakiwa na umri wa miaka mitano. Wawili hawa walikulia katika mji mmoja nchini Argentina na wakabaki kuwa marafiki hata baada ya Messi kwenda kufanya majaribio Barcelona.


Wawili hawa walijitambulisha rasmi kuwa wapenzi mwaka 2009 na sasa wana watoto wawili.


Comments