DAVID                  MOYES (pichani kulia) anataka kurejea tena Everton                  iwapo Roberto Martinez (pichani kushoto) atatimuliwa                  kutokana na mwenendo mbovu msimu huu.
            Bodi                  ya Everton itakutana wiki hii kujadili hatma ya Martinez ambaye                alijiunga na timu hiyo mwaka 2013 kuchukua nafasi ya Moyes                aliyekwenda Manchester United.
            Moyes amewaambia                watu wake wa  karibu kuwa atapendelea kurejea Everton                licha ya kuwaniwa na Celtic na Aston Villa.
            
Comments
Post a Comment