Dakika 452, hakuna goli wala assist – Lionel Messi kwenye kiwango kibovu kuliko wakati wowote wa maisha yake kwenye soka



Dakika 452, hakuna goli wala assist – Lionel Messi kwenye kiwango kibovu kuliko wakati wowote wa maisha yake kwenye soka

Je presha ya kufunga goli namba 500 imemkamata Lionel Messi? 

 Mshindi  wa mara ya 5 wa Ballon d'Or amekuwa kwenye kiwango cha chini zaidi kwenye maisha. 

Messi alikuwa anakaribia kutimiza magoli 500 kwa klabu na nchi yake akiwa na miaka 28 wakati alipofunga goli la 499 akiwa Argentina katika mechi vs Bolivia. 

Hata hivyo, ameshindwa kufunga katika mechi 5 mfululizo – dakika zaidi ya 400 – ameshindwa pia hata kutoa assist. 

Huu ndio ukame mkubwa zaidi kwa Messi tangu mwaka 2010. 

  Lakini dakika 452 bila kufunga goli ndio kipindi kirefu zaidi kwake tangu alipoanza kucheza soka la ushindani. 

Kushuka kwa Messi pia kumeungana na kudondoka kwa Barcelona tukielekea mwishoni mwa msimu. 

Goli lake la mwisho kufunga akiwa na Barcelona lilikuwa katika robo fainali ya Champions League mchezo wa pili vs Arsenal. 
Tangu wakati huo, Barca walipoteza uongozi wao goli 2 baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Villareal, kisha wakaja kufungwa kwenye El Clasico pamoja na Madrid kuwa pungufu, wakapoteza tena vs Sociedad na sasa wamekuja kutolewa na Atletico Madrid katika Champions League. 

Ushindi wao pekee ulikuwa dhidi ya vijana wa Diego Simeone ambao walicheza pungufu zaidi ya dakika 60 – ushindi huu kwa sasa haumanishi chochote. 



Comments