Manager wa Real Madrid Zinedine Zidane anasema Cristiano Ronaldo ni 'mchezaji bora duniani' baada ya kikosi chake kuichakaza Wolfsburg kwa bao 3-0 kwenye mchezo wao wa marudiano war obo fainali ya Champions League.
Real Madrid walikuwa kwenye wakati mgumu kufatia kipondo cha bao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza. Hat-trick ya Ronaldo iliishuhudia Madrid ikifuzu kwenda nusu fainali ya ya mashaindano hayo.
Baada ya mchezo, Zidane akasema: "Cristiano Ronaldo anaonesha yeye ni mchezaji wa aina gani. Ni mchezaji bora ulimwenguni na amefanya kitu kinachomfanya aonekane ni mchezaji maalumu."
"Lakini anahitaji timu nzima kufanya yote hayo, na tunachohitaji kufanya ni kuzungumza kile ambacho kimefanywa na wachezaji kwa pamoja. Lakini si kila mchezaji anaweza kufunga magoli matatu hilo liko wazi."
Comments
Post a Comment