CHINA KUFANYA KUFURU KWENYE SOKA, YAJIANDAA KUJENGA VIWANJA 60,000 NCHI NZIMA



CHINA KUFANYA KUFURU KWENYE SOKA, YAJIANDAA KUJENGA VIWANJA 60,000 NCHI NZIMA

AMINI usiamini. China imepania kujenga viwanja 60,000 vya soka katika kipindi cha miaka sita ijayo katika harakati zake za kuifanya nchi hiyo kuwa kati ya mataifa makubwa duniani katika mchezo wa soka kufikia mwaka 2050.

Hayo yamo katika mapendekezo ya ripoti ya Serikali kuhusu mwelekeo wa soka ya nchi hiyo kufikia mwaka huo.

Ripoti hiyo imeelezea pia mipango ya kuimarisha idadi ya wachezaji na watoto wanaocheza soka kufikia milioni 50 pamoja na kuwa na klabu zenye hadhi ya kimataifa.

Aidha Rais Xi Jinping amenukuliwa akisema kuwa atakuwa mwenye furaha kubwa iwapo timu ya taifa ya China itafuzu tena kucheza Kombe la Dunia, na hata kutwaa ubingwa, huku akichagiza jitihada za kuhakikisha wanakuwa wenyeji wa michuano hiyo.


Comments