CHELSEA YAKOMAA NA KUPATA SAINI YA HENRIKH MKHITARYAN WA BORUSSIA DORTMUND



CHELSEA YAKOMAA NA KUPATA SAINI YA HENRIKH MKHITARYAN WA BORUSSIA DORTMUND

GAZETI la Ujerumani la Bild limeeleza kwamba Klabu ya Chelsea kwa mara nyingine tena inajiandaa kupeleka maombi ya kumsajili straika wa Borussia Dortmund, Henrikh Mkhitaryan licha ya ofa yake ya pauni milioni 46.8 kukataliwa kiangazi kilichopita.

Chelsea imekolezwa mzuka na habari kwamba staa huyo wa kimataifa wa Armenia mwenye umri wa miaka 27 tayari anatafuta nyumba katika Jiji la London.

Kuingia kwa Chelsea kuwania saini ya straika huyo aliyepiga mabao 11 na kupika 18 katika mechi 29 za Bundesliga msimu huu, kunaelezwa kuwa changamoto kwa majirani zao Arsenal ambao nao wapo katika harakati za kumfukuzia.


Comments