CHELSEA NA WAZIMU WA KUTAFUTA MBADALA WA JOHN TERRY, YAMTAKA SERGIO RAMOS KWA PAUNI MIL 63



CHELSEA NA WAZIMU WA KUTAFUTA MBADALA WA JOHN TERRY, YAMTAKA SERGIO RAMOS KWA PAUNI MIL 63

CHELSEA inataka kuandika rekodi ya uhamisho England kwa kumsajili beki wa Real Madrid, Sergio Ramos kwa kitita cha pauni milioni 63.5.

Kwa mujibu wa jarida la michezo la kila wiki la Hispania, Don Balon, Chelsea iko tayari kulipa dau hilo kwa ajili ya uhamisho wa beki huyo, ambao unamaanisha mwisho wa John Terry.

Ramos mwenye miaka 30, ambaye mara zote amekuwa akitajwa kama mmoja wa mabeki bora duniani, ameitumikia Real Madrid kwa miaka 11 sasa, lakini Chelsea inaamini dau hilo rekodi linaweza kuwashawishi vigogo hao wa La Liga kumwachia.

Staa huyo wa kimataifa wa Hispania alikuwa katikati ya tetesi za uhamisho kiangazi kilichopita ambapo Manchester United ilijaribu kumsajili bila mafanikio.


Terry amebainisha kutaka kuondoka Stamford Bridge mwisho wa msimu, lakini Antonio Conte anataka kufanya mazungumzo na nahodha huyo wakati atakapochukua rasmi timu kiangazi hiki.


Comments