CHELSEA imekuwa ikihusishwa na uhamisho wa Paul Pogba na Leonardo Bonucci wa Juventus, na Mkurugenzi Mkuu wa miamba hiyo ya Serie A, Beppe Marotta amebainisha kuwa dili linaweza kufanyika kati ya klabu hizo mbili.
Marotta ameripotiwa akisema kuwa anataka kufanya biashara na Chelsea kiangazi hiki kufuatia kuwasili kwa kocha Antonio Conte katika klabu hiyo ya Stamford Bridge.
Conte alishinda mataji matano ya Serie A akiwa mchezaji wa kiungo Juve kabla ya kuiongoza kushinda mataji matatu mengine akiwa kocha, na Marotta amesisitiza kuwa anafurahia kumuona Mtaliano huyo akipata kazi katika Premier League.
"Sisi na Chelsea tunaheshimiana," aliiambia Radio Rai. "Tunaona fahari kwamba Conte sasa ni kocha wao… Ni jambo ambalo tunaweza kujivunia, kama sisi tulijitoa mhanga miaka mitano iliyopita wakati tulipomkabidhi kuiongoza Juventus… Natumaini tutaweza kufanya kazi pamoja katika soko la usajili."
Hata hivyo, Marotta, haraka akathibitisha kwamba uhusiano wa heshima hautakwenda mbali kiasi cha kutosha kuwauzia Pogba.
Comments
Post a Comment