KIUNGO wa Chelsea raia wa Hispania, Cesc            Fabregas, ameeleza wazi kuwa hataki kuona Tottenham ikishinda            taji la Premier League msimu huu.
        Tottenham imeachwa pointi tano nyuma ya            Leicester baada ya kuibamiza 4-0 Stoke City Jumatatu usiku, na            kubaki kuwa timu yenye uwezekano zaidi wa kuzima ndoto za            vinara hao wa ligi.
        Hata hivyo, akizungumza akiwa mchambuzi            mwalikwa katika televisheni ya Sky Sport wakati wa mechi ya            Spurs na Stoke, Fabregas alisema angependa Leicester            kukamilisha historia yao kwa kushinda taji hilo.
        Fabregas aliwahi kuichezea Arsenal, ambayo            ni mpinzani mkubwa wa Spurs jijini London, kabla ya kuhamia            Chelsea ambayo pia inatoka katika jiji hilo.
        
Comments
Post a Comment