BUFFON KA-POST UJUMBE TWITTER KUHUSU RANIERI NA LEICESTER


BUFFON KA-POST UJUMBE TWITTER KUHUSU RANIERI NA LEICESTER

Ranieri-Gigi

Gianluigi Buffon amehibitisha kwamba yeye ni professional, hiyo ni baada ya kufurahia mafanikio aliyoyapata kocha wake wa zamani Claudio Ranieri kwa kuiwezesha Leicester City kucheza michuano ya Champions League msimu ujao.

Msimu ujao Buffon anaweza akakutana na Leicester City na anafurahia hilo, siyo kwasababu timu za England zimekuwa hazina makali kwenye ligi ya mabingwa Ulaya lakini atakachofurahia ni kukutana na muitaliano mwenzake.

Buffon ameshacheza mashindano yote makubwa na kushinda mataji makubwa ambayo kila mchezaji anatamani kutwaa lakini golikipa huyo mkongwe hajawahi kutwaa taji la klabu bingwa Ulaya.

Alikaribia kunyanyua ndoo hiyo mara mbili lakini mara zote timu yake ilipoteza kwenye mchezo wa fainali, alipoteza fainali dhidi ya AC Milani mwaka 2003 kabla ya kuchapwa na Barca kwa mara nyingine kwenye mchezo wa fainali mwaka uliopita.

Buffon amecheza Juventus kwa muda mrefu na amewahi kuwa chini ya Claudio Ranieri lakini kocha huyo yeye amekuwa akizunguka kwenye bara la Ulaya kufundisha timu tofauti. Wawili hao walikuwa pamoja msimu ambao Juve ilimaliza ikiwa nafasi ya tatu msimu wao wa kwanza tangu warejee Serie A kufatia kashfa ya upangaji matokeo 'Calciopoli'.

Huu ndiyo ujembe alioandika Gianluigi Buffon kwenye account yake ya twitter kuikaribisha Leicester City kwenye michuano ya UEFA Champions Legue.

Leicester-uefa

Leicester-uefa 1



Comments