Bayern Munich imefuzu hatua ya nusu fainali ya Champions League kwa mara ya tano mfululizo baada ya kuitupa nje ya mashindano klabu ya Benfica ya Ureno.
Benfica ilikubali mkichapo cha bao 1-0 kwenye mchezo wa kwanza ugenini, walifufua matumaini baada ya Raul Jimenez kupasia kamba kwenye mchezo wa marudiano wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani.
Arturo Vidal alichomoa bao hilo kisha Thomas Muller kuongeza bao la pili na kuiweka mbele Bayern kwa magoli 2-1.
Free-kick ya Talisca ilijaa moja kwa moja wavuni baada ya Javi Martinez kunusurka kulimwa kadi nyekundu kutokana na mchezo wake usio wa kiungwana.
Bayern boss Pep Guardiola will join Manchester City this summer and the two clubs could meet in the last four when the draw is made on Friday.
Boss wa Bayern Pep Guardiola atajiunga na Manchester City kipindi cha majira ya joto na klabu hizo mbili huenda zikakutana kwenye nusu fainali wakati draw ya kutafuta timu zitakazoumana kwenye hatua ya nusu fainali ya Champions League.
Takwimu muhimu;
- Thomas Muller amefikisha magoli 36 kwenye michuano ya Champions League, magoli 10 zaidi ya mchezaji mwingine wa kijerumani.
- Arturo Vidal 'back-to-back' kwenye mashindano ya klabu bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu November 2013.
- Benfica wamefunga magoli manne kwa vichwa kwenye Champions League, Bayern pekee ndiyo wanawazidi wakiwa wamefanya hivyo mara sita (6).
- Bayern wamefika hatua ya nusu fainali ya Champions League mwa mara ya sita ndani ya misimu saba iliyopita.
- Benfica wamefunga goli kwa free-kick ya moja kwa moja kwa mara ya kwanza tangu wafanye hivyo October 2011 (dhidi ya Basel).
Comments
Post a Comment