BARCELONA imeripotiwa kumfukuzia kipa wa Bayer Leverkusen, Bernd Leno kwa ajili ya kuziba nafasi ya Marc-Andre ter Stegen, ambaye anaelezwa kuwa njiani kuondoka Bundesliga katika usajili wa kiangazi hiki na kuhamia La Liga au Premier League.
Hata hivyo, Barca inatakiwa kuchangamka kama inataka kumpata Leno kwa bei nafuu.
Kipa huyo Mjerumani aliye chaguo la pili, kwa mujibu wa mkataba wake wa sasa unaofikia kikomo Aprili 30, klabu inayomtaka italazimika kulipa euro milioni 16.25.
Zimebaki siku chache kufika Aprili 30, hivyo Barca inatakiwa kukimbia na muda, kwani Leverkusen inaweza kupandisha thamani ya kipa huyo mara mbili zaidi.
Kipa huyo wa miaka 24 ambaye kwa mujibu wa The Sun yuko mguu ndani mguu nje baada ya kutoelewana na kocha wake, Roger Schmidt, amemvutia pia kocha wa Tottenham Hotspur, Mauricio Pochettino lakini kuna uwezekano mdogo wa kukubali kwenda kuwa nyuma ya Hugo Lloris.
Barcelona inaonekana kuwa chaguo bora kutokana na kutarajiwa kumruhusu Ter Stegen kuondoka mwisho wa msimu, na hivyo kupambana na Claudio Bravo kwa ajili ya kuanza kikosini.
Comments
Post a Comment