BARCELONA SAFARI IMEWADIA, YAPIGIGWA 2-0 NA ATLETICO MADRID NA KUTOLEWA CHAMPIONS LEAGUE ...BAYERN NAYO YASONGA
Barcelona imeshindwa kulinda ushindi wake wa 2-1 ilioupata nyumbani kwake dhidi ya Atletico Madrid wiki iliyopita na sasa imeaga michuano ya Ligi ya Mabingwa.
Miamba hiyo ya Hispania ikakubali kichapo cha 2-0 katika mchezo uliochezwa Jumatano usiku na kufungasha virago kwa jumla ya bao 3-2.
Mabao yote ya Atletico yamefungwa na Antoine Griezmann dakika ya 36 na 88.
Atletico sasa inaungana na Manchester City, Real Madrid na Bayern Munich katika hatua ya nusu fainali.
Bayern Munich imevuka kwenda nusu fainali baada ya kutoka sare ya 2-2 na Benfica na hivyo kuvuka kwa jumla ya 3-2 kufuatia ushindi wa 1-0 katika mchezo wa kwanza.
ATLETICO XI: Oblak, Juanfran, Godin, Lucas, Filipe Luis, Augusto (Savic 93), Gabi, Saul, Koke, Griezmann (Correa 90), Carrasco (Partey 74)
BARCELONA XI: Ter Stegen, Alves (Sergi Roberto 64), Mascherano, Pique, Alba, Busquets, Rakitic (Arda Turan 64), Iniesta, Neymar, Suarez, Messi
Comments
Post a Comment