ARSENE WENGER amekiri kuwa ndoto za kutwaa ubingwa wa Premier League zimeyeyuka na kuziacha kwa Leicester City na Tottenham baada ya sare ya 3-3 dhidi ya West Ham Jumamosi jioni, na sasa anatazama timu zinazowafuata nyuma katika msimamo.
Baada ya Leicester City kuilamba Sunderland 2-0 Jumapili, sasa Arsenal iko pointi 13 nyuma ya vinara vinara hao wenye michezo 33 dhidi ya 32 ya kikosi cha Wenger.
Katika mchezo wa Jumamosi ndani ya dakika 35 Arsenal ilikuwa mbele kwa mabao mawili ya Mesut Ozil na Alexis Sanchez kabla Andy Carroll kupiga mabao matatu 'hat-trick' na kuiweka mbele West Ham. Baadae Laurent Koscielny alisawazisha, lakini Arsenal ilishindwa kupata ushindi.
"Nafasi ya tatu katika ligi, pointi 59. Na hapo sipo tulipotaka kuwapo, na nafasi ya ubingwa tumeifanya wenyewe kuwa ngumu sana.
"Tunapaswa kuendelea kuwa na matumaini, huwezi kujua – kama vile ambavyo inabidi kuangalia nyuma yetu. Timu zinatukimbiza na tunapaswa kumaliza juu iwezekanavyo," alisema Wenger alipoulizwa nafasi yake katika mbio za ubingwa.

Comments
Post a Comment