RATIBA ya hatua ya mtoano ya timu 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika imetoka ambapo Mabingwa wa Tanzania, Yanga wamepangwa kucheza na GD Esperanca ya Angola.
Yanga imeangukia katika michuano hiyo ambayo ni ya pili kwa ukubwa Afrika baada ya kufungwa na Al Ahly ya Misri kwa mabao 2-1 Jumatano usiku na kutupwa nje ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 3-2. Mechi ya kwanza walitoka 1-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika hatua hiyo, Yanga wataanzia nyumbani kati ya Mei 6 na 8 kabla ya kuifuata GD Esperanca katika mchezo wa marudiano kati ya Mei 17 na 18.
Mechi nyingine: Al Ahli Tripoli vs Misr Makkassa; Mamelodi Sundowns vs Medeama SC; Al Merreikh vs Kawkab Marrakesh; TP Mazembe vs Stade Gabesien; Etoile du Sahel vs CF Mounana na MO Bejaia vs Esperance Tunis.
Comments
Post a Comment