ATLETICO MADRID YAENDELEA KULISONGESHA LA LIGA, YAIFUNGA MALAGA 1-0 ...kocha Diego Simeone 'apigwa benchi' jukwaani
KOCHA wa Atletico Madrid, Diego Simeone amejikuta akimalizia kipindi cha pili jukwaani katika mechi ya La Liga waliyoshinda 1-0 dhidi ya Malaga katika dimba la Vicente Calderon Jumamosi jioni baada ya mpira wa pili kurushwa uwanjani.
Matokeo yalikuwa 0-0 wakati mechi ikielekea mapumziko, ambapo Malaga walionekana kufanya shambulizi la kushtukiza, lakini refa Antonio Mateu Lahoz akasimamisha mchezo baada ya mpira wa pili kuingia dimbani.
Haikujulikana mara moja nani aliyerusha mpira huo dimbani, lakini refa alionekana akizungumza na Simeone wakati timu zikitoka nje kwa mapumziko, na wakati mechi ilipoanza kipindi cha pili kocha huyo alikaa jukwaani.
Sheria za La Liga zinaeleza kwamba kocha mkuu atawajibika kwa tabia zitakazojitokeza katika benchi lake, hivyo Simeone anaweza kuadhibiwa iwapo aliyerusha mpira uwanjani alikuwa mmoja wa wasaidizi wake.
Atletico ilishinda mechi hiyo kwa bao la dakika ya 62 lililofungwa na mtokea benchi Angel Correa kwa shuti kutoka umbali wa yadi 20.
Angel Correa akisharehekea bao lake
Correa (kushoto) akishangilia na kocha msaidizi German Burgos
Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone akishangilia huku akiwa jukwaani baada ya kutolewa kipindi cha pili
Comments
Post a Comment