Pep Guardiola ana kazi nzito ya kuutumia vema mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa ili kuepukana na nuksi ya kukomea nusu fainali tangu alipoanza kuikochi Bayern Munich.
Kibarua hicho kigumu kinakuja baada ya Bayern kupokea kisago cha bao 1-0 kutoka kwa Atletico Madrid katika wa mchezo wao kwanza Jumatano usiku.
Hii ni mara ya tatu mfululizo kwa Guardiola kutinga hatua ya nusu fainali akiwa na Bayern Munich ambapo mara mbili zilozopita, alikomea hatua hiyo ya nusu fainali.
Timu hizo zinarudiana Ujerumani Jumanne ijayo katika mchezo unaotarajiwa kuwa mgumu kupindukia.
Bao pekee la Atletico lilifungwa na Saul Niguez kunako dakika ya 11.
Saul Niguez akishangilia bao lake
Saul akipongezwa na wenzake
Kocha wa Atletico Diego Simeone akitoa maelekezo
Fernando Torres aliikosesha Atletico bao la wazi dakika ya 75
Comments
Post a Comment