ARSENE Wenger amepuuza stori kuwa amemfanya staa wa Leicester City, raia wa Algeria, Riyad Mahrez, kuwa lengo lake kuu katika mabadiliko makubwa anayotarajia kufanya katika kikosi chake kiangazi hiki, ikiwamo 'kufagia' wachezaji walioshuka kiwango.
Inadaiwa Wenger aliachia nafasi ya kumsajili Mahrez mwenye thamani ya pauni milioni 25 sasa Januari 2014 kabla ya kujiunga na Leicester kwa ada ya pauni 400,000 akitokea Le Havre inayoshiriki Ligue 2 ya Ufaransa.
Bosi huyo wa Gunners amekiri kuwa moja ya sababu za kumwacha wakati huo ilikuwa ni kukwepa kukosolewa kwamba 'amechukua mchezaji asiye na jina badala ya kulipa pauni milioni 40 kwa mchezaji mwenye jina kubwa'.
Klabu kibao kubwa za Ulaya ikiwamo Barcelona, zinamtaka staa huyo wa miaka 25, lakini Wenger amewaeleza rafiki zake kwamba kumsajili kiungo huyo mchezeshaji ndiyo kipaumbele chake.
Alipoulizwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari kama anamtaka nyota huyo, Wenger alijibu: "Habana na hata kama namtaka siwezi kusema lolote kwa muda huu".
Comments
Post a Comment