ARSENE WENGER ameripotiwa kujiandaa kumpa nafasi katika kikosi cha kwanza kinda Gedion Zelalem kiangazi hiki.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 19 anacheza kwa mkopo katika klabu ya Rangers ya Scotland msimu huu na ameonyesha uwezo mkubwa akiwa na kikosi hicho cha Mark Warburton.
Zelalem aliyezaliwa Ujerumani na wazazi kutoka Ethiopia, ambaye kwa sasa ana uraia wa Marekani, aligunduliwa na msaka vipaji wa Arsenal, Daniel Karbassiyoon nchini Marekani wakati akiichezea Olney Rangers katika michuano ya Dallas Cup na Wenger ameweka matumaini makubwa kwa kinda huyo.
Mikel Arteta, Mathieu Flamini na Tomas Rosicky wanatarajiwa kuondoka Emirates kiangazi hiki na gazeti la Telegraph limesema kwamba hilo linatoa nafasi kwa Zelalem kupandishwa kikosi cha kwanza.

Comments
Post a Comment