ARSENAL YAWEKA REHANI MBIO ZA UBINGWA, YABANWA 3-3 NA WEST HAM ...pata matokeo ya mechi zote za Premier League
Zikiwa zimesalia mechi sita ligi kumalizika, Arsenal imejikuta ikiwa pointi 11 nyuma kwa vinara Leicester City baada ya kulazimishwa sare ya 3-3 dhidi ya West Ham katika mchezo mkali wa Premier League.
Arsenal itabidi ijilaumu kwa kushindwa kuondoka na pointi tatu baada ya kukubali kupoteza uongozi wa bao 2-0 kutokana na magoli ya Ozil na Sanchez yaliyokuja dakika ya 18 na 35.
Mshambuliaji Andy Carroll akawa nyota wa mchezo kwa kupiga hat-trick pale alipofunga magoli ya kusawazisha dakika ya 44 na 45 kabla hajaifungia West Ham goli la kuongeza dakika ya 52.
Sentahafu Laurent Koscielny akaikoa Arsenal kwa kuisawazishia dakika ya 7o.
Ili kunyakua ubingwa, Arsenal anahitaji angalu kushinda michezo mitano kati ya sita iliyobakia na kuomba Leicester pia ifungwe michezo mitano, Tottenham ifungwe michezo miwili.
Matokeo ya mechi zote zilizochezwa mapema Jumamosi ni:
West Ham United 3 - 3 Arsenal
Aston Villa 1 - 2 AFC Bournemouth
Crystal Palace 1 - 0 Norwich City
Southampton 3 - 1 Newcastle United
Swansea City 1 - 0 Chelsea
Watford 1 - 1 Everton
West Ham (3-4-2-1): Adrian 5; Tomkins 5.5 (Emenike HT, 6), Reid 7, Ogbonna 6.5; Antonio 6, Kouyate 6.5, Noble 7.5, Cresswell 7; Payet 6.5, Lanzini 6.5; Carroll 8.
Arsenal (4-2-3-1): Ospina 6; Bellerin 6, Gabriel 6, Koscielny 7, Monreal 5; Elneny 6.5 (Giroud 68, 5), Coquelin 5.5 (Ramsey 61, 5); Sanchez 6, Ozil 5.5, Iwobi 7; Welbeck 5 (Walcott 85).
Andy Carroll wa West Ham (kushoto) akifunga goli la tatu
Carroll anashangilia bao lake la tatu

Comments
Post a Comment