ANTONIO CONTE KUFANYA USAJILI CHELSEA KUENDANA NA MFUMO WA 4-2-4 ...wamo Antoine Griezmann na Javier Pastore,



ANTONIO CONTE KUFANYA USAJILI CHELSEA KUENDANA NA MFUMO WA 4-2-4 ...wamo Antoine Griezmann na Javier Pastore,
Italy manager                Antonio Conte will arrive at Stamford Bridge once his Euro                2016 campaign is over 
KOCHA mpya wa Chelsea, Antonio Conte anautolea macho usajili wa nyota wenye majina makubwa watakaofiti katika mfumo wake wa kushambulia wa 4-2-4 msimu ujao.

Conte ambaye ataachia kibarua chake kama kocha wa timu ya taifa ya Italia na kujiunga na Chelsea baada ya Euro 2016, amevutiwa na mafanikio ya Leicester City inayotumia mfumo huo wa kushambulia msimu huu.

Pamoja na kuwa na sifa ya kujihami, Conte anaamini anaweza kupeleka soka la kuburudisha Stamford Bridge na kubadili mwelekeo wa timu kutoka zama za Jose Mourinho.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mirror, Conte atakuwa 'busy' katika soko la usajili kiangazi hiki, huku mastraika kama Antoine Griezmann na Zlatan Ibrahimovic wakiwa chaguo lake kuu katika safu ya ushambuliaji.

Conte pia anaaminika kufungia kazi usajili wa Radja Nainggolan au Javier Pastore katika safu ya kiungo, huku Leonardo Bonucci akimtamani kwa ajili ya kuimarisha ngome.

Kocha huyo wa zamani wa Juventus, pia anatarajiwa kuwabakisha mastaa wengine kama Eden Hazard na Diego Costa, licha ya kuwa wameonekana kutetereka viwango vyao msimu huu.


Comments