WEST HAM UNITED imeripotiwa kufanya mawasiliano na Lyon ya Ufaransa juu ya uwezekano wa kumtwaa mshambuliaji wao nyota, Alexandre Lacazette katika usajili wa kiangazi hiki.
Mfaransa huyo mbunifu dimbani, amekuwa akihusishwa pia na timu nyingine kubwa England kama Arsenal na Liverpool, na Hammers wanaweza kuwazidi kete wapinzani wao hao katika Premier league kwa kulipa pauni milioni 31.
Huu ni mpango kabambe kwa Hammers, lakini kwa mujibu wa L'Equipe, inadhaniwa kwamba Lacazette atazingatia kujiunga nao kama watafuzu kucheza Champions League msimu ujao na si vinginevyo.
Kikosi hicho chini ya Slaven Bilic kipo pointi mbili nyuma ya mstari wa nafasi ya nne – ya mwisho katika orodha ya timu za kufuzu Champions League inayoshikiliwa na Manchester City yenye pointi 51, na inaweza kufanikiwa kama itachanga karata zake vyema.
Comments
Post a Comment