WEST HAM KUKARABATI UWANJA OLYMPIC STADIUM


WEST HAM KUKARABATI UWANJA OLYMPIC STADIUM
UONGOZI wa klabu ya Westham United umethibitisha taarifa za kutaka kuufanyia ukarabati uwanja wa Olympic Stadium kwa minajili ya kuwa na uwezo wa kuingiza watazamaji wengi zaidi ya ilivyo sasa.

Taarifa za mtandao kutoka ndani ya uongozi zimebainisha kuwa, pindi ukarabati huo ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuingiza jumla ya watazamaji 60,000.

Wagonga nyundo wamepanga kuutumia uwanja wa Statford kama dimba lao la nyumbani baada ya kuweko Upton Park kwa miaka 112.

Dimba hilo la Upton Park lina uwezo wa kuingiza watazamaji 54,000.


Hatua ya Westham kutaka kuongeza idadi ya watazamaji ni kutokana na kuona inatimiza mahitaji ya ongezeko la bei la tiketi iliyoongezwa kwa pauni 30 hivyo wamepanga kuongeza watu zaidi ya 6,000 kwa kuongeza viti kutoka idadi ya 54,000 kwa uwanja wa Upton Park.


Comments