WACHEZAJI 8 AMBAO KLABU ZAO ZA ZAMANI ZINGEPENDA KUWARUDISHA


WACHEZAJI 8 AMBAO KLABU ZAO ZA ZAMANI ZINGEPENDA KUWARUDISHA

Warejeshwe

Dunia inakwenda kasi sana na maisha yanabadilika sana, kuna baadhi ya wachezaji waliondoka kwenye vilabu vyao lakini leo vilabu hivyo vinawatamani wachezaji hao kutokana na viwango vyao kuendelea kuimarika kila inapoitwa leo. Inawezekana vilabu hivyo vinajilaumu kwanini viliamua kuwaachia wachezaji hao kutimka kutokana na kuvifaidisha vilabu ambavyo wanavitumikia kwa sasa.

Wafuatao ni wachezaji 8 ambao huenda klabu zao za zamani zinatamani ziwarejeshe kundini kwa sasa.

8. Robert Lewandowski (Borusia Dortmund)

ZAGREB, CROATIA - DECEMBER 09: Robert Lewandowski              celebrates scoring the second Bayern Munich goal during the              UEFA Champions League Group F match between GNK Dinamo              Zagreb and FC Bayern Munchen at Maksimir Stadium on December              9, 2015 in Zagreb, Croatia. (Photo by Alexander              Hassenstein/Bongarts/Getty Images)

Lewandowski ni mshambuliaji wa kiwango cha juu na iliwaumiza sana mashabiki wa Dortmund kumshuhudia akiondoka mwaka 2014 na kujiunga na wapinzani wao wakubwa Bayern Munich. Tangu hapo mshambuliaji huyo raia wa Poland amezidi kuwa bora na kuwa miongoni mwa ma-striker bora duniani kwa sasa. Borussia Dortmund wamerejea kwenye reli msimu huu na wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

Bado wangependa kuwa na Lewandowski na huenda pengine angewasaidia kutwaa ubingwa wa Bundesliga.

7. Romelu Lukaku (Chelsea)

NORWICH, ENGLAND - DECEMBER 12: Romelu Lukaku of              Everton celebrates scoring his team's first goal during the              Barclays Premier League match between Norwich City and              Everton at Carrow Road on December 12, 2015 in Norwich,              United Kingdom. (Photo by Stephen Pond/Getty Images)

Mshambuliaji huyu raia wa Ubelgiji alisajiliwa na Chelsea mwaka 2011. Akatolewa kwa mkopo misimu miwili baadaye kwenye klabu za West Bromwich Albion na Everto. Hata baada ya kufunga jumla ya mabao 33 ndani ya hiyo misimu miwili akiwa nje ya Chelsea kwa mkopo, kocha wa kipindi hicho Jose Mourinho bado hakushawishikia kumpa nafasi kinda huyo kwenye kikosi chake cha kwanza.

Hali hiyo ilimfanya Lukaku kuamua kujiunga na Everton kwa uhamisho wa kudumu, lakini kawasa Chelsea wanatamani kumrejesha Lukaku kwenye kikosi chao kutokana na kiwango chake kuwa cha hatari kwa sasa.

6. Kevin de Bruyne (Chelsea)

Warejeshwe 3

Kevin De Bruyne ni mchezaji mwingine ambaye anakumbukwa sana na mashabiki wa Chelsea baada ya kumwachia aondoke na kwasasa anakipiga kwenye klabu ya Manchester City. Alisajiliwa kutoka klabu ya Genk mwaka 2012 na kupelekwa kwa mkopo kwenye klabu ya Werder Bremen na baadaye Wolfsburg.

Msimu wake wa mwisho akiwa Wolfsburg ulikuwa ni wa mafanikio kutokana na kuwa miongoni mwa viongo wachezeshaji bora barani Ulaya. Man City walimuona na kuamua kumsajili kipindi kilichopita cha usajili wa majira ya joto kwa ada ya uhamisho wa pound milioni 55.

Kushuhudia kiwango chake anachokionesha kwa sasa kwenye kila mchezo, kunaifanya Chelsea kutamani kuwa nae tena kwenye kikosi.

5. Javier Hernandez (Manchester United)

Warejeshwe 4

Javier Hernandez a.k.a Chicharito alikuwa kwa mkopo kwenye kikosi cha Real Madrid. Chicharito aliamua kuondoka Old Trafford baada ya kutokuwa na uhakika wa kucheza kufuatia Van Gaal kuchukua nafasi ya ukocha mkuu kwenye klabu ya Manchester United.

Kwasasa anakipiga Ujerumani kwenye klabu ya Bayer Leverkusen, nyota huyo wa Mexico amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu na kuisaidia klabu yake ya Bundesliga baada ya kuifungia mabao 22 kwenye michuano yote. United wamekuwa na tatizo la ufungaji msimu huu na huenda wanatamani kumrejesha Hernandez Old Trafford.

4. Luis Suarez (Liverpool)

Luis Suarez of FC Barcelona during the Joan Gamper              Trophy match between FC Barcelona and Leon F.C. at Camp Nou              on august 18, 2014 in Barcelona, Spain(Photo by VI Images              via Getty Images)

Msimu wa 2013-14 ni msimu ambao Liverpool ilikaribia kutwaa ubingwa wa Premier League tangu ifanye hivyo mwaka 1990.

Shukrani zimwendee Suarez, Liverpool ilikuwa inakaribia kutwaa taji la Premier League msimu wa 2013-14. Alikuwa ni mchezaji muhimu kwenye msimu huo akifanikiwa kupachika mabao 31 kwenye msimu mzima. Lakini hatimaye waliishia kuwa nafasi ya pili na Suarez kuamua kujiunga na Barcelona msimu uliofuata. Tangu kipindi hicho, Suarez ametwaa La Liga, CopaDel Rey, Champions League pamoja na FIFA Club World Cup akiwa na miamba hiyo ya Catalan.

Bila shaka hata kidogo, Liverpool wanatamani kumrudisha Suarez ili kuwasaidia kushinda ubingwa wa Premier League.

3. Paul Pogba (Manchester United)

Warejeshwe 6

Paul Labile Pogba ni miongoni mwa wachezaji waliozalishwa kwenye academy ya Manchester United. Kukosa kwake nafasi ya kucheza kulimfanya nyota huyo wa Ufaransa atimkie kwenye klabu ya Juventus na tangu ajiunge na mabingwa hao wa Italy jamaa hajarudi nyuma tena.

Ufundi wake kwenye eneo la katikati ya uwanja unavitoa udenda vilabu vikubwa duniani na vikotayari kulipa kiasi chochote cha pesa ili kumnasa. Pogba huenda angekuwa msaada mkubwa wakati huu ambapo United inapambana kurejea kwenye ubora wake, klabu hiyo inatamani kufanya lolote ili kumrudisha mcheaji huyo.

2. Mesut Ozil (Real Madrid)

Warejeshwe 7

Kiungo huyu wa kijerumani amekuwa kwenye kiwango kizuri msimu huu, akiwa anaongoza kwa assists kwenye Premier League. Nyota huyu mwenye miaka 27 ameshasaidia timu yake kufunga mabao 17 hadi sasa na amekuwa msaada mkubwa kwa kutengeneza magoli kwenye kikosi cha Arsenal. Alikuwa ni mchezaji muhimu kwenye klabu ya Real Madrid na miamba hiyo ya Hispania bado haijapata mrithi sahihi aliyezipa nafasi ya Ozil tangu ajiunge na Arsenal.

Real Madrid wanatamani wapate fursa ya kumsajili tena bingwa huyo wa kombe la dunia.

1. Cristiano Ronaldo (Manchester United)

Warejeshwe 8

United wakotayari kulipa kiasi chochote cha pesa kumrejesha Ronaldo Old Trafford. Nyota huyo wa Ureno alikuwa na wakati mzuri akiwa Manchester United, kiwango chake kiliivutia klabu ya Real Madrid kumsajili lakini uwezo huo wote aliunesha akiwa na 'mashetani wekundu'.

Man United inahitaji msaada wa mchezaji wa aina yake hivyo wanatamani kumuona winga huyo akiwa ndani ya uzi mwekundu.



Comments