LICHA ya timu kuboronga na kukiri kuwa atakuwa amefeli msimu huu kama atashindwa kumaliza katika timu tatu za juu, Louis van Gaal haonyeshi dalili za kubwaga manyanga Manchester United msimu huu.
"Sijawahi kuhisi kuwa kwenye shinikizo… Ninafanya ninachopaswa kufanya. Kila siku wakati tunapopoteza au kutupwa nje ya Euro league au ligi nyingine, basi unaweka swali. Lakini kwanini?
"Nina mkataba wa miaka mitatu na kipimo cha mafanikio ni miaka mitatu. Lengo letu lilikuwa ni kufika 'top three' kwa sababu tunataka kufanya vizuri zaidi kuliko mwaka uliopita. Lakini matarajio yanaweza kuwa makubwa mno.
"Unapaswa kuchambua hali ilivyo na jinsi gani unapaswa kufanya kazi," alisema.
Comments
Post a Comment