Louis van Gaal amekiri kuwa kinda wa Machester United Marcus Rashford ana kila kitu anachostahili kuwa nacho mshambuliaji mahiri.
Kocha huyo wa United ameyasema hayo baada ya kinda huyo kuifungia timu yake bao pekee kwenye ushindi wa 1-0 dhidi ya mahasimu wao Manchester City.
Bao la dakika ya 16 la Rashford lilitosha kupunguza pengo la pointi kwenye Premier League kati ya United na City ambapo sasa Manchester United imeachwa kwa pointi moja tu.
Van Gaal akakiri kuwa chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 18 alijihakikishia namba mara tu alipomchezesha mchezo wake wa kwanza mwezi uliopita. Hadi sasa Rashford kishatupia mabao matano katika michezo nane aliyocheza.
Marcus Rashford akipongezwa na Louis van Gaal
Rashford akiitungua Man City dakika ya 16
Rashford akipongezwa na wachezaji wenzake
Comments
Post a Comment