TIMU 5 ZILIZOWAHI KUTWAA UBINGWA WA LIGI ZIKIWA HAZIPEWI NAFASI


TIMU 5 ZILIZOWAHI KUTWAA UBINGWA WA LIGI ZIKIWA HAZIPEWI NAFASI

Ndoo 1

Wakati ligi mbalimbali zikiwa zinaelekea ukingoni huku baadhi ya ligi hizo zikiwa tayari zimeshawapata mabingwa wake, gumzo kubwa kwa sasa li kwenye ligi ya England maarufu kama EPL ambayo hadi sasa Leicester City ndiyo wapo kileleni mwa ligi huku wapenda soka wengi wakishangazwa na kiwango kinachooneshwa na timu hiyo.

Leicester ingawa bado haijatwaa ubingwa lakini haikuwa ikifikiriwa kuwepo kwenye mbio za timu za juu ambazo zinawania ubingwa wa ligi msimu huu. Lakini tarati mechi zinazidi kupungua na Leicester City bado inaendelea kukaa kileleni mwa EPL na haitakuwa ajabu kama timu hiyo inayonolewa Claudio Ranieri itabeba ndoo ya Premier League.

Shaffihdauda.co.tz inakuletea timu tano za ligi tofauti Ulaya ambazo zimewahi kutwaa ubingwa wa ligi huku zikiwa hazipewi nafasi ya kufanya hivyo.

Nottingham Forest (1977-78)

Ndoo 2

Kocha wa wakati huo wa Nottingham Forest Brian Clough alikuwa ni kocha bora wa Premier League kuwahi kutokea. Watu wengi walikuwa wakidhani Nottingham ingeshuka daraja baada ya kupanda mwishoni mwa msimu wa 1976-77. Iliwashangaza wengi, Clough kwa msaada mkubwa wa golikipa wa England Peter Shilton, makinda kama Tony Woodcock na Kenny Burns waliweza kucheza msimu huo huku wakipoteza mechi tatu kati ya 42 na kutwaa taji la ligi ya England.

FC Kaiserslautern (1997-98)

Ndoo 3

Otto Rehhagel alikiongoza kikosi cha Kaiserslautern baada ya timu hiyo kupanda kucheza ligi ya Ujerumani na watu wengi walitarajia kuishuhudia timu hiyo kupambana kuzuia isishuke daraja. Lakini Kaiserslautern walimshangaza kila mmoja, Olaf Marschall alifunga mabao 21 kwenye michezo 24 aliyoichezea Kaiserslautern na kwa msaada wa wachezaji wengine kama vijana kama Michael Ballack na Andreas Brehme, Kaiserslautern ilitwaa ubingwa wa Bundesliga  na kuwa timu ya kwanza kutwaa kikombe cha ligi baada ya kupanda daraja.

Lazio Roma (1999-2000)

Ndoo 4

Msimu wa 1999-2000 kwenye Serie A kulikuwa na upinzani mkali kati ya Lazio dhidi ya Juventus kwenye kuwania ubingwa wa ligi hiyo hadi siku ya mwisho ya msimu. Sven Gorak Eriksson alikuwa anakinoa kikosi cha Lazio wakati huo kikiwa na wachezaji wa kiwango cha juu kama Alessandro Nesta, Pavel Nedved na Juan Sebastian Veron. Juventus walipoza mchezo wao wa mwisho kwa goli 1-0 dhidi ya Peruggia na kuwafanya Lazio kutwaa ubingwa wa Serie a baada ya miaka 25.

Montpellier (2011-12)

Ndoo 5

Mshambuliaji wa sasa wa Arsenal Olivier Giroud alikuwa na msimu mzuri akiwa kwenye kikosi cha Montpellie na kufanikiwa kufunga mabao 21 huku akipika mengine 9. Kinda Younes Belhanda alifanya vizuri pia msimu huo akicheza nyuma ya Giroud. Rene Girard aliwatumia vyema wachezaji wake na kutwaa taji la Ligue 1, akimaliza pointi tatu mbele ya Paris Saint Germain.

Atletico Madrid (2013-14)

Ndoo 1

La Liga imekuwa ikitawaliwa na Real Madrid pamoja na FC Barcelonakwa kipindi cha miaka kadhaa. Haikuwa kazi rahisi kuzizuia timu hizi kutwaa taji la ligi lakini Diego Simeone ameweza kufanya hivyo. Diego Costa akipachika mabao 27 kwenye msimu huo, Koke akitengeneza mabao 13, kiwango kikubwa cha Diego Godin na uwepo wa Thibaut Coutois katikati ya milingoti mitatu kulimsaidia Simeone kuzipindua Barca na Madrid na kutwaa ubingwa wa ligi.



Comments