SHIRIKISHO la Soka Italia (Federazione Italiana Giuoco Calcio - FIGC) – Federcalcio kimsingi limethibitisha safari ya Antonio Conte kuhamia Chelsea baada ya kutangaza kuwa anaacha majukumu yake kama kocha wa timu ya taifa ya Italia maarufu kama Azzurri.
Mkataba wa Conte utafikia ukomo baada ya Euro 2016 na alitarajiwa kuongeza, kabla ya Chelsea kutaka huduma yake.
Tetesi zilichukua nafasi kwa wiki kadhaa sasa kwamba amekubali kufanya kazi na klabu hiyo ya Stamford Bridge, na angelifahamisha Federcalcio wakati wowote.
Lakini sasa safari ya Conte kwenda Chelsea imethibitishwa na Rais wa Federcalcio, Carlo Tavecchio mwenye umri wa miaka 45 baada ya kueleza kuwa anaondoka Italia.
"Antonio Conte amenieleza muda wake na Italia utamalizika baada ya Euro," alisema Tavecchio.

Comments
Post a Comment