Shanta Ronaldo: Kijana wa Kidenmark aliyedata na CR7, Husafiri kutoka Denmark -Spain kila mara kujaribu kukutana na Ronaldo
Kijana mmoja wa kidenmark na mahaba yaliyopitiliza kwa Cristiano Ronaldo, na amekuwa akitumia fedha nyingi kujitengeneza afanane nae na mara kwa mara amekuwa akisafiri kwenda jijini Madrid kujaribu kuonana na Ronaldo.
Kijana huyo anayejitambulisha kwa jina la 'Shanta Ronaldo' husafiri kutoka Denmark mpaka Hispania kumsubiri Ronaldo kwa masaa 6 wakati mreno huyo akiwa mazoezini, kabla ya kusafiri tena kurudi kwao Denmark.
Imefikia hatua kijana huyo hujitangaza kwamba amesaini kuitumikia Real Madrid na yeye na Ronaldo ni wachezaji wa timu moja.
Hata familia ya kijana huyu sasa inamuita 'Cristiano Ronaldo' na hivi karibuni tu ametoka kwenye trip ya pamoja na mama yake kutoka Spain kujaribu kukutana na Ronaldo.
Kijana huyu ametumia fedha nyingi sana kujaribu kujitengeneza afanane na Ronaldo kimwili mpaka kimavazi na tabia.
Wakati akiwa anamsubiri Ronaldo amalize kufanya mazoezi, huwa anaenda kupozi kwenye gari ya Ronaldo na kupiga picha – Shanta pia hupata chakula chake katika mgahawa wa Santiago Bernabeu.
Shanta anasema: "Popote, CR7 atakapoenda, nitakuwa nae, hata yeye mwenyewe anajua."
Anapokuwa nyumbani kwao, Shanta humuigiza Ronaldo kupiga picha na mdogo wake wa kiume – kama ambavyo Ronaldo hupiga picha na mwanae. '.
Shanta tayari ameanza kupata umaarufu mtandaoni – kupitia Twitter tayari ana followers 17,000.
Pale anapokosa nafasi ya kuonana na Ronaldo wakati anaposafiri kwenda Spain – basi huishia kujaribu japo kukutana na wachezaji wengine wa Madrid – na anamtaja beki Pepe kama rafiki yake. .
Akiongea na gazeti la Mirror la Uingereza, alisema: 'Najaribu kumtembelea Ronaldo mara kwa mara. Kwasasa napanga utaratibu wa safari yangu nyingine kwenda Spain."
Katika siku ya wanawake duniani – Shanta alitweet picha ya mama mzazi wa Cristiano Ronaldo na kuandika – 'Mom I wish you had a beautiful International Women's Day'.
Inafahamika kwamba Shanta amekuwa akiiga mpaka staili ya uchezaji ya Ronaldo.
Comments
Post a Comment