SAMATTA AING’ARISHA STARS UGENINI



SAMATTA AING'ARISHA STARS UGENINI

Maguli 2

Mbwana Samatta akivaa kitambaa cha unahodha kwa mara ya kwanza, amekiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kupata ushindi wa goli 1-0 ugenini dhidi ya Chad kwenye mchezo wa Group G kuwania nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika inayotarajiwa kufanyika mwaka 2017 nchini Gabon.

Mbwana Samatta amefunga goli hil kipindi cha kwanza akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Farid Musa goli ambalo limedumu hadi dakika 90 za mchezo huo.

Stars imefikisha pointi 4 baada ya kucheza michezo 3, matokeo hayo yanaifanya Stars ifikishe idadi sawa ya pointi na Nigeria 'The Super Eagles' lakini Stars ipo mbele ya Nigeria kwa mchezo mmoja. Nigeria itakutana na Misri kwenye mchezo wa kundi ilo siku ya Ijumaa.

Stars itacheza mchezo wake wa marudiano dhidi ya Chad siku ya Jumatatu March 28 mwaka huu kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Msimamo wa Group G unaongowa na Misri yenye pointi 6 ikifatiwa na Nigeria na Tanzania zenye pointi 4 lakini Nigeria ikishika nafasi ya pili kwa tofauti ya magoli wakati Chad ikiwa ya mwisho bila pointi. Tanzania na Chad zimecheza mechi 3 mechu moja mbelea ya Misri na Nigeria.

Group G Matokeo ya mechi nyingine za kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa mechi ambazo tayari zimemalizika yapo kama ifuatavyo:

Guinea-Bissau 1-0 Kenya

South Sudan 1-2 Benin



Comments