SABABU 5 SIMBA KUSHINDA DHIDI YA COASTAL UNION KWENYE UWANJAWA WA MKWAKWANI


SABABU 5 SIMBA KUSHINDA DHIDI YA COASTAL UNION KWENYE UWANJAWA WA MKWAKWANI
Wachezaji wa Simba wakimpongeza mchezaji mwenzao Hamisi              Kiiza aliyefunga bao la pili kwenye mchezo dhidi ya Coastal              Union
Wachezaji wa Simba wakimpongeza mchezaji mwenzao Hamisi Kiiza aliyefunga bao la pili kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union

Klabu ya Simba SC iliendelea kufanya vyema kwenye mechi zake za ligi baada ya kushinda kwamara nyingine kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga mchezo wake wa ligi dhidi ya Coastal Union na kuwa timu pekee ya Dar es Salaam kupata ushindi kwenye uwanja huo dhidi ya Coastal msimu huu.

Ushindi huo haukuja kama bahati kwa Simba, shaffihdauda.co.tz imekuandalia sababu tano zilizofanya Simba ipate matokeo ya ushindi kwenye uwanja wa Mkwakwani dhidi ya Coastal Union ambao wamekuwa wagumu kufungika kwenye uwanja wao wa nyumbani dhidi ya timu vigogo kutoka Dar.

Morali ya ushindi wa mechi zilizopita

Kwa sasa timu ya Simba ina ari ya juu sana kutokana na mwendelezo wa matokeo mazuri wanayoendelea kuyapata kwenye michezo yao ya ligi tangu kutua kwa Mayanja kwenye kikosi chao. Simba imerejea kwenye mbio za ubingwa na wachezaji, viongozi, wanachama na mashabiki wanaamini timu yao ni miongoni mwa timu tatu zinazowania ubingwa msimu huu.

Kitu kizuri ni Simba kuendelea kushinda mechi zake, wapinzani wao Azam na Yanga wao wameendelea kuwa na viporo kutokana na ratiba ya ligi kubadilishwa kuzipa nafasi timu hizo kushiriki michuano ya kimataifa. Endapo Simba itaendelea kufanya vizuri bila kujali wapinzani wake wanafanya nini bila shaka itakuwa inajitengenezea mazingira mazuri ya kutwaa ndoo ya ligi msimu huu.

Kiu ya ubingwa

Simba haijabeba kombe la ligi msimu wa tatu sasa mfululizo, kombe hilo limekuwa likitua mikononi mwa Azam na Yanga huku Simba wakiwa wanalisikia na kuliangalia tu. Kibaya zaidi wamekuwa hawapati hata nafasi ya pili ya kuwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa nafasi ambayopo msimu huu haipo kutokana na kurejea kwa kombe la FA ambalo mshindi wake atakwenda kushiriki michuano ya kombe la shirikisho Afrika.

Wachezaji wengi wa Simba hwajawahi kulinyanyua kombe la ligi kuu Tanzania bara, kutokana na wachezaji wengi kuwa ni vijana ambao wamepandishwa kutoka kikosi B hivyo hawakuwahi kulitwaa taji hilo wakati timu yao ilipofanya hivyo. Wachezaji wengine ni wa kigeni ambao wamekuja wakati ambao timu hiyo haijachukua kombe la Vodacom tangu wao wafike.

Vipigo walivyopata 'vigogo' kutoka Coastal kwenye uwanja wa Mkwakwani

Uwanja wa Mkwakwani Tanga umekuwa mchungu kwa vigogo vya ligi baada ya Coastal kuvunja utawala wao. Coastal ndiyo timu ya kwanza kwenye ligi kuzifunga Azam na Yanga ambazo zilikuwa hazijafungwa tangu kuanza kwa ligi msimu huu. Coastal imefanya hivyo kwenye uwanja wa Mkwakwani, ilianza kuifunga Yanga kwa bao 1-0 kisha Azam ikalala pia kwa bao 1-0.

Simba walikuwa wanalitambua hilo, kwamba Coastal wanaamini wanaweza kufanya lolote kwenye uwanja wao wa nyumbani kwasababu tayari wameshafanya hivyo kwa timu mbili za Dar zilitotangulia kwenye uwanja huo. Simba wakaingia uwanjani wakiwa na lengo moja tu la kuifunga Coastal kwenye uwanja wao ambao wanajidaia.

Simba haina historia ya matokeo mazuri dhidi ya Coastal Union

Huu ni ushindi wa tatu kwa Simba dhidi ya Coastal Union katika mechi nane za ligi ambazo timu hizo zimecheza hivi karibuni, ikumbukwe msimu huu Simba imeshinda mechi zote dhidi ya Coastal Union. Kwa maana hiyo, Simba haikuwa na rekodi nzuri ya kupata matokeo mbele ya Coastal Union hasa kwenye uwanja wa Mkwakwani.

Historia ya Simba kutofanya vizuri kila inapokutana na Coastal iliifanya Simba kuingia uwanjani ikiwa na lengo la kupata matokeo licha ya Coastal kuwa mkiani kwa ligi, benchi la ufundi la Simba lilikuwa likitambua ugumu uliopo mbele yao hasa walipoangalia historia yao dhidi ya 'waosi wa kaya'

Mashabiki

Simba ilihamasisha mashabiki wake kusafiri kwenda Tanga kuishangilia timu yao itakapokuwa ikicheza dhidi ya Coastal Union kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Mashabiki waliitikia wito huo na kwa kiasi kikubwa walijaa kwenye uwanja huo, Simba walikuwa wanajua umuhimu wa mashabiki waliosafiri kutoka sehemu mbalimbali za nchi kwenda Tanga kui-support timu.

Kitu pakee ambacho Simba kama timu walitakiwa kuwalipa mashabiki hao ni ushindi ndiyo maana walipambana kuhakikisha wanashinda.

Ushindi wa Simba dhidi ya Coastal umewafanya mashabiki hao wasahau gharama walizotumia kutoka mikoa tofauti kwenda Tanga kuishangilia timu yao tofauti na matokeo ya ushindi, Simba ingekuwa imewakatisha tama mashabiki wake waliojaa kwenye uwanja wa Mkwakwani.



Comments