Urafiki wa Ronaldo na mcheza kick boxer Badr Hari umekua mkubwa sana ndani ya mwaka mmoja sasa ambapo amefikia hatua hadi ya kumpa nyumba yake ambayo ipo kwenye ghorofa kubwa huko jijini New York.
Habari hizi za Ronaldo kumpa nyumba rafiki yake zimekuja baada ya kutokea ishu za jina la Ronaldo kutumika vibaya kwenye kesi za kampuni moja inayouza nyumba kwenye majiji mbalimbali Ulaya na Marekani.
Kampuni hiyo ya Proto Enterprises inasemekana imetumia jina Ronaldo kwenye mambo yao ya kesi kuhusu nyumba ambayo inamataatizo kisheria na kusema Ronaldo pia alihusika kwa wakati fulani kwenye ishu ya manunuzi.
Upande wa Ronaldo umetoa statement kwamba jina la Ronaldo limetumika sivto kwa muda kidogo na wawakilishi wa kampuni ya Proto kwenye kesi zao nchini Italy. Hivyo basi wanataka lisihusishwe mara moja.
Kama unakumbuka story hizi za Ronaldo kununua nyumba kwenye ghorofa kubwa lilipo jijini New York ambapo baadhi ya nyumba za humo ndani zinamilikiwa na mwanasiasa Donald Trump.
Hii ni picha ya nyumba ambayo inaripotiwa Ronaldo kwamba amempa rafiki yake wa karibu raia wa Morocco.
Comments
Post a Comment