RONALDINHO AINGIA KWENYE HEADLINES ZA USAJILI MPYA


RONALDINHO AINGIA KWENYE HEADLINES ZA USAJILI MPYA

ronaldinho2

Kaka wa Ronaldinho ambaye pia ni meneja wake Roberto Assis ameweka wazi kwamba kunauwezekano mkubwa mteja wake akahamia ligi ya Marekani 'Major League Soccer' au akaelekea China kucheza kwenye 'Chinese Super League' ambako ndipo kutakuwa mwisho wa maisha yake ya soka.

"Mwisho wa soka lake huenda ikawa ni Major League Soccer ya Marekani au Chinese Super League nchini China" Assis aliiambia UOL.

Nyota huyo wa kibrazil anamiaka 36 alifanikiwa kushinda tuzo ya Ballon d'Or mara mbili, Champions League na World Cup, ni baadhi ya mataji makubwa ambayo amewahi kushinda kwenye maisha yake ya soka huku akiwa hajacheza soka la ushindani tangu alipomaliza adhabu ya kufungiwa miezi miwili na klabu ya Fluminense mwezi September mwaka jana.



Comments