PICHA 60: MHE. NAPE NNAUYE ALIPOKUTANA NA WANAMUZIKI WA DANSI NA KUAHIDI KUREJESHA MUZIKI WA DANSI …ataka vyama vya muziki vijisafishe, aahidi kuifumua Cosota
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye Jumatatu mchana alikutana na wadau na wanamuziki wa dansi katika ukumbi wa Vijana Social Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano huo mkubwa, Nape alisikiliza kero mbali mbali za wasanii wa muziki wa dansi na kuahidi kuwa atapambana kurejesha heshima ya muziki wa dansi.
Pamoja na kujibu hoja mbali mbali za wanamuziki wa dansi, Nape akaamuru iundwe kamati ya watu 11 itakayowasaliana naye maja kwa moja katika kutafuta njia nzuri ya kutatua baadhi ya kero na baadae kupeleka mrejesho kwa wanamuziki.
Nape akasema kamati hiyo itakuwa ni kiunganishi cha muda kati yake na wanamuziki wa dansi.
Miongoni mwa mambo aliyoahidi Nape ni pamoja na kuzipunguzia bendi kodi zisizo na lazima wakati zinapofanya maonyesho yao kwenye kumbi mbali mbali.
Nape aliyekuwa akishangiliwa mara kwa mara na wanamuziki, akaahidi pia kuifumua COSOTA (Chama cha Hatimiliki) pamoja na kuvisafisha vyama vya muziki kikiwemo Chamudata.
"Hatutasaidia chama chochote kabla ya kuvisafisha," alisema Nape na kushangiliwa kwa nguvu hasa pale alipoongeza: "Vyama hivi vinaonyesha vina walakini na ndio maana wanamuziki wengi hawavifuati."
Waziri huyo wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pia akaahidi kuwakutanisha wanamuziki wa dansi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli.
"Nitahakikisha muziki wa dansi unarejesha heshima yake, muziki wa dansi ndiyo muziki wa ukweli lakini wanamuziki wake wanakufa masikini," alisema Nape ambaye pia alihidi kurejesha matamasha na mashindano ya muziki wa dansi.
Moja ya kero kubwa na iliyolalamikiwa sana kwa Mheshimiwa Nape ni suala la bendi kutakiwa kumaliza maonyesho yao saa 6 za usiku, jambo aliloahidi kulishughulikia.
"Hili lipo kwa mujibu wa sheria, lakini tutaangalia namna ya kulitatua maana kwa kweli watu wengi wanaokwenda dansi wanaingia ukumbini saa 6 za usiku, sasa unapotaka muda huo ndiyo muziki uzimwe inakuwa ni tatizo," alitiririka Mheshimiwa Nape.
Baadae Nape aliyekuwa akiongea mbele ya vingozi wa Shirikisho la Muziki la Vyama vya Muziki Tanzania, CHAMUDATA (Chama Cha Muziki wa Dansi Tanzania) na BASATA (Baraza la Sanaa la Taifa), akataja majina ya kamati ya watu 11 aliotaka iundwe.
Nape akataka yeyote mwenye tatizo na mjumbe yeyote wa kamati hiyo iliyopendekezwa na viongozi wa Shirikisho la Muziki la Vyama vya Muziki Tanzania, Chamudata na Basata, aseme na ataondolewa.
Miongoni mwa majina yaliyounda kamati hiyo ni Waziri Ali, Hamza Kalala, Kida Waziri, Asha Baraka, Ally Chocky, Abdallah Mgonahazilu, Edna Pambamoto, Said Mdoe na Hassan Msumari (Katibu wa Chamudata) ambaye wanamuziki walilipinga jina lake na nafasi yake ikachukuliwa na Khalid Chokoraa.
Zifuatazo ni picha 60 za mkutano huo wa Mheshimiwa Nape na wanamuziki wa dansi.
Mheshimiwa Nape akisikiliza hoja za wanamuziki wa dansi
Mwanamuziki mkongwe Abuu Omar
Nyoshi akisalimiana na Asha Baraka
Shaaban Dede akitoa hoja
Hassan Msumari katibu wa CHAMUDATA
Wanamuziki wakisimama pale Nape alipowasili ukumbini
Hussein Jumbe
Jado FFU
Ally Jamwaka wa Sikinde
Edna Pambamoto na William Kaijage
Mwimbaji wa Kalunde Band
Matei na Kanku Kelly
Francis Kaswahili na Anna Mwaole
Dephin Mununga na Keppy Kiombil
Nyoshi na Khalid Chokoraa
Khamis Dacota na Chaz Baba
Juma Mbizo na Said Kibiriti
Kida Waziri "Stone Lady" na Asha Baraka "Iron Lady"
John Kitime akiandaa vidokezo muhimu
Wanamuziki wakongwe wakimsikiliza Nape
Malu Stonch wa FM Academiaa
Mama Kitenge (kushoto) na Edna Pambamoto
Nyoshi na Hamza Mapande "Dogo White" wa Twanga Pepeta
Adoplh Mbinga na Hajj BSS wa Twanga Pepeta (kulia)
Waziri Ali wa Njenje (kushoto) akiwa na Abdul Misambano wa TOT
Mjusi Shemboza wa Sikinde (kushoto) na Bonphace Kachele
Mule Mule FBI wa BMM Band na Balatee wa FM Academia
Kushoto ni mwimbaji Liston Maina
Mwinjuma Muumin na mwandishi Khadija Khalili
Mzee Makassy (kushoto) akimsikiliza Nape kwa makini
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye akizungumza na wanamuziki wa dansi
Mheshimiwa Nape akisisitiza jambo
Marlon Linje na Innocent Nganyagwa
Ado November rais wa Shirikisho la Vyama vya Muziki Tanzania
Wanamuziki wengi walijitokeza
Nyoshi el Saadat kiongozi wa FM Academia
Patcho Mwamba na Totoo Ze Bingwa nao walikuwepo
Kulia ni Rashid Pembe
Mwanahabari Peter Mwendapole
Dekanto Bass (kushoto) na Pitchou Meshaa wote kutoka Akudo
Mpiga solo Rama Karenga
Rama Pesambili meneja wa Akudo Impact
Mwimbaji Hassan Rehani Bitchuka
Rogart Hegga na Ally Chocky
Mwimbaji Roshy Mselela
Bosi wa Ruby Band
Mwanamuziki mkongwe Salum Zahoro
Kushoto ni Ally Star wa TOT
Maria mdau wa muziki wa dansi kutoka Italia (kushoto) akiwa na mtangazaji Mwinyiami Maftah "Stazo"
Kushoto ni Taji Mbaraka
Nape akiwa meza kuu na viongozi wa Basata, Chamudata na shirikisho la muziki
Jimmy Chika mhariri wa Dimba
Waandishi wa habari
Wadau na wanamuziki wakimsikiliza Nape
Ally Chocky na Adolph Mbinga
Wanamuziki waliofurika Vijana Social Hall
William Kaijage
Comments
Post a Comment