Wimbo "Nimpe Nani" wa Isha Mashauzi ulitia fora Ijumaa usiku katika onyesho la Mashauzi Classsic huko Muscat, Oman.
Onyesho hilo lililofanyika Sohar Garden, likashuhudia wimbo huo ukirudiwa mara mbili baada ya mashabiki kuomba urudiwe mara kwa mara.
Isha Mashauzi ndiye aliyetoka jasho zaidi katika onyesho hilo baada ya kuimba jumla ya nyimbo 12.
Waimbaji wengine waliotesa vilivyo kwenye onyesho hilo ni Saida Ramadhan, Asia Mzinga, Zubeida Malick na Naima Mohamed.
Tupia macho picha 13 za onyesho hilo la Mashauzi Classic ambao tayari wameshakwea pipa kurejea nyumbani.
Mashabiki wa Muscat wakiselebuka na goma la Mashauzi
Naima Mohamed
Mgeni Kisoda akingurumisha bass gitaa
Isha Mashauzi akitupia masauti yake
Wasanii wa Mashauzi jukwaani
Isha akiwa na mmoja wa mashabiki
Zubeida Malick
Asia Mzinga
Hapa ni Isha alipokuwa akiingia ukumbini
Saida Mashauzi
Isha Mashauzi
Mashabiki waliofurika Sohar Garden
Comments
Post a Comment