KOCHA ajaye Manchester City, Pep Guardiola ametoa maelekezo kwa klabu hiyo kumpiga bei beki wake, Vincent Kompany.
Bosi huyo anayemalizia mkataba wake Bayern Munich kabla ya kujiunga rasmi na City mwisho wa msimu, haoni nafasi ya beki huyo Mbelgiji katika kikosi anachotaka kukijenga Etihad.
Mhispania huyo amelenga kusaini majina makubwa katika safu ya ulinzi kama John Stones na Aymeric Laporte, na haoni pa kumuweka Kompany, hata katika safu ya kikosi cha akiba.
Kwa mujibu wa The Sun, tayari Guardiola amewasiliana na Mkurugenzi wa Soka City, Txiki Begiristain na kumwambia ampige bei beki huyo wa kati aliye majeruhi.
Comments
Post a Comment