PAUL SCHOLES ATAKA WATATU WASAJILIWE MANCHESTER UNITED ...ni Luka Modric, Raphael Varane na Paul Pogba



PAUL SCHOLES ATAKA WATATU WASAJILIWE MANCHESTER UNITED ...ni Luka Modric, Raphael Varane na Paul Pogba

Gwiji wa Manchester United Paul Scholes amependekeza klabu yake hiyo ya zamani iwasajili Luka Modric, Raphael Varane na Paul Pogba katika dirisha lijalo la usajili kama kweli timu hiyo inataka kurejesha mafanikio yake barani Ulaya.

Mabadiliko kadhaa yanatarajiwa kufanyika Manchester United kwa kusajili nyota wapya pamoja na kuwafungisha virago wachezaji waliochemsha, hii ikiwa ni pamoja na benchi la ufundi linaloongozwa na Louis van Gaal.

Inaaminika kocha huyo Mholanzi atatimuliwa mwishoni mwa mismu huku nafasi yake ikihusishwa kwa karibu na kocha wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho.

Scholes, ambaye aliichezea United kati ya mwaka 1992 na 2013, amesema wachezaji hao ni sahihi katika kutibu baadhi ya maeneo yaliyoiangusha timu msimu huu.

Raphael Varane anacheza beki ya kati wakati Luka Modric na Paul Pogba ni wakali wa safu ya kiungo.
Manchester United legend Paul Scholes has                  identified the three players he would bring to Old                  Trafford
Gwiji wa Manchester United  Paul Scholes amependekeza wachezaji watatu wa kusajiliwa Old Trafford
Scholes would make an attempt to sign Luka                    Modric     And                    his Real Madrid team-mate Raphael Varane
Scholes angependa nyota wa Real Madrid Luka Modric (kushoto) na Raphael Varane (kulia) watue Old Trafford
He                  would also try to entice Juventus midfielder Paul Pogba                  back to Old Trafford during the summer window
Scholes pia anataka United imrejeshe Paul Pogba
Pogba                  was on the books at Manchester United between 2009 and                  2012 before he left the club on a free transfer
Pogba alikuwa Manchester United kati ya mwaka 2009 na 2012 kabla hajaondoka kwa uhamisho huru




Comments