OZIL AIPA ARSENAL SHARTI GUMU ILI KUBAKI EMIRATES


OZIL AIPA ARSENAL SHARTI GUMU ILI KUBAKI EMIRATES

Mesut 2

Mesut Ozil anaweza kuondoka Arsenal mwishoni mwa msimu ikiwa Arsene Wenger ataendelea kubaki kukinoa kikosi hicho.

Mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Ujerumani amekuwa katika kiwango bora msimu huu lakini ameonekana kuchoshwa na timu hiyo kutokana na kukosekana kwa makombe, lakini vile vile mikakati thabiti kwa ajili ya kuleta makombe klabuni hapo, hivyo kutoa msimamo wake wa kubaki endapo Wenger ataondoka.

Tetesi zinaeleza kwamba, kiungo huyo yuko mbioni kurejea Uhispania hasa kweny e klabu ya Atletico Madrid ambayo imeonesha nia ya wazi ya kumuhitaji endapo ada ya uhamisho na malipo mengine vitawezekana.

Klabu nyingine zilizoonesha nia ni Sevilla na Valencia.



Comments