NYOSHI HATAKI KUITWA RAIS, ASEMA SASA YEYE NI “SIR NYOSHI” …kisa? utitiri wa marais



NYOSHI HATAKI KUITWA RAIS, ASEMA SASA YEYE NI "SIR NYOSHI" …kisa? utitiri wa marais

Kiongozi wa FM Academia, Nyoshi el Saadat amesema hataki tena kuitwa cheo cha rais na badala yake sasa atambulike kama Sir Nyoshi.

Nyoshi amesema yeye ndiye aliyeasisi jina la rais kwa upande wa wanamuziki mwaka 1997, lakini sasa wimbi la wasanii kujiita marais limevuka mpaka na hivyo ameamua kuachana na jina hilo.

"Marais wamekuwa wengi sana, sasa tutakuwa marais wangapi? Sitaki tena hilo jina, kuanzia leo nataka nitambulike kama Sir Nyoshi," alisema Nyoshi Ijumaa iliyopita ndani ya Mango Garden Kinondoni.


Comments