N'GOLO KANTE ASEMA LEICESTER CITY KWANZA ‘ARSENAL’ BAADAE



N'GOLO KANTE ASEMA LEICESTER CITY KWANZA 'ARSENAL' BAADAE

WAKATI kukiwa na tetesi kwamba kiungo N'golo Kante anafukuziwa na klabu za Juventus na Arsenal, mwenyewe amesema kilicho kwenye akili yake kwa sasa ni timu yake ya Leicester City.

Kante mwenye umri wa miaka 24, ni mmoja wa wachezaji waliosajiliwa na Leicester msimu huu akitokea Caen ya nyumbani kwao Ufaransa kwa dau lililoripotiwa kuwa pauni milioni 5.6.

"Nimeweka umakini wangu kwa Leicester tu. Tuna msimu wa kumaliza, vinginevyo sisikii chochote," aliwaambia waandishi katika kambi ya timu ya taifa ya Ufaransa Jumanne wiki hii. "Hakuna klabu iliyonifuata moja kwa moja, sitaki kuweka umakini sana kwa uvumi. Premier League ni ligi inayonifaa," alisema.

Kante ametoa mchango mkubwa kwa Leicester, na kuifanya kuwa katika nafasi ya kuandika historia ya kushinda Premier League kwa mara ya kwanza tangu ianzishwe mwaka 1884.


Comments