MTANZANIA MWINGINE ANAYECHEZA ENGLAND APIGA HODI STARS (Video)


MTANZANIA MWINGINE ANAYECHEZA ENGLAND APIGA HODI STARS (Video)
Abbas Pira akiwakwenye uwanja wa Stamford Bridge uwanja              unaomilikiwa na klabu ya Chelsea ya London England
Abbas Pira akiwakwenye uwanja wa Stamford Bridge uwanja unaomilikiwa na klabu ya Chelsea ya London England

Inawezekana mafanikio ya mtanzania Mbwana Samatta yamekuwa kichocheo cha watanzania wengine wanaocheza nje ya nchi kurejea nyumbani huku wakiwa na shauku kubwa ya kutaka kukipiga kwenye timu yao ya taifa.

Tatizo hapa ni profile zao kutokuwa wazi hususan wale walioondoka Tanzania wakiwa vijana wadogo, Abbas Pira ni mtanzania mzaliwa wa barabara ya tatu jijini Tanga, motto wa tajiri anayemiliki visima vya mafuta jijini humo Gulam Pira mchezaji wa zamani wa Coastal Union msimu wa 2002/03 na 2004 akiwa chini ya aliyekuwa kocha mkuu wakati huo marehemu Zakaria Kinanda.

Pira akiwapanga vizuri mabeki wake kuhakikisha timu              yake hairuhusu bao
Pira akiwapanga vizuri mabeki wake kuhakikisha timu yake hairuhusu bao

Abbas aliondoka Tanzania msimu wa mwaka 2006 akiwa na umri wa miaka 17 na kwenda nchini Uingereza kwa ajili ya masomo ya juu. Akiwa London Uingereza, Abbas Pira aliendelea kucheza soka kwenye mitaa mbalimbali ya jiji hilo.

Akiwa huko alichezea vilabu kama Hillington FC, FC Wibledon pamoja na Kilburn FC, baadaye Pira alijiunga na kituo cha kukuza vipaji cha Football CV Academy kilichopo kwenye mji wa Northampton kisha baadaye kwenda kufanya majaribio katika klabu za Chelsea, Birmingham City MK Dons.

Pira akijiandaa vyema golini mwake kuzuia hatari
Pira akijiandaa vyema golini mwake kuzuia hatari ya mpira wa kona

Sports Xtra ya Clouds FM imezungumza na Abbas Pira kutaka kujua sababu zilizomfanya kurejea nchini pamoja na kushindwa kakwe kucheza kwenye vilabu vikubwa nchini England.

www.shaffihdauda.co.tz: Nipe historia yako kwa ufupi

Abbas Pira: Mimi naitwa Abbas Pira nilizaliwa Tanga February 20, 1988 nina umri wa miyaka 28 sasa, mimi ni goalkeeper nimecheza sana mtaani nilianza mpira timu moja ilikuwa inaitwa Mzambarauni Stars baadaye Coastal Union walinichukua kufanya nao mazoezi nilikuwa mdogo sana kipindi hicho.

Marehemu Zakaria Kinanda akaanza kunifundisha na Joseph Lazaro hawa ndiyo walichangia kipaji changu sana ndiyo nikaanza kufundishwa mpira na kina marehemu Saidi Mhando alishawahi cheza Yanga.

2005-2006 nilikwenda England huko mimi nilianza na timu za semi professional ambayo nilicheza kwenye Middlesex League nikacheza timu kama Hillingdon FC, Willesdon Costatine, AFC Wembley, Tokynton, Manor FC, Kilburn FC nikashinda mataji mengi baada hapo nikachukuliwa na Academy ya Football CV ambayo ilikuza wachezaji wengi kama captain msaidizi wa Manchester United wa sasa hivi Chriss Smalling baada hapo academy walivyoona nimefanya vizuri wakanipeleka trial Chealsea FC.

Pira akiwa ameunyaka mpira mpira kwenye moja ya mechi              zake huko barani Ulaya
Pira akiwa ameunyaka mpira mpira kwenye moja ya mechi zake huko barani Ulaya

www.shaffihdauda.co.tz: Ukiwa nje ya nchi, ulichezea timu gani?

Abbas Pira: Nilicheza Stanford Bridge halafu nikaenda Birmingham City, Meyton Orient Coalcheste FC,  MK Dons baada hapo nilipata offer ya MK Dons lakini kulitokea tatizo kwenye kibali cha kazi kwasababu Tanzania haikuwa ndani ya timu 70 bora kwenye viwango vya FIFA, kupata kazi ya mpira England lazima Tanzania iwe 70 bora.

Nina experience ya kutosha nilishasomea ukocha nilivyokuwa academy ninauwezo wakufundisha timu yoyote ya under 17,  nimekuja Tanzania kwa muda nimepata offer kazi hapa nyumbani ila sijajua bado nitacheza timu gani maana kwasababu nitakuwa nyumbani nataka kucheza league mwakani niweze kutunza kipaji changu bado natafuta timu.

www.shaffihdauda.co.tz: Unalizungumziaje soka la Tanzania

Abbas Pira: Soka la kitanzania limeendelea sana sasahivi tuna viwanja vizuri vingi tu wachezaji wananunuliwa nje makocha wazuri wachezaji wanalipwa vizuri sasahivi tunauwezo wankuzifunga timu kubwa tumewekeza vizuri soka la vijana.

www.shaffihdauda.co.tz: Kitu gani ambacho ukiwa nje ya nchi, hutoweza kukisahau?

Abbas Pira: Kituambacho sitaweza kusahau siku ambayo nilialikwa kufanya majaribio Chelsea FC kwenye uwanja wao wa Stanford Bridge maana nimeanza mbali mpira hadi kufika Chelsea ni hatua kubwa .

247891_10150667619435145_5185834_n

www.shaffihdauda.co.tz: Ni wachezaji gani wanao kuvutia ndani na nje ya nchi? Na unashabikia timu gani ndani na nje ya nchi?

Abbas Pira: Mchezaji ambaye ananivutiya ni Zinedine Zidane ila kwa goalkeeper ni Fabien Barthez 'ndiyo jina langu la mtaani'

Hapa tanzania mchezaji anayenivutiya ni Kelvin Yondani, mimi ni shabiki wa Coastal Union nje ya nchi ni Manchester United.

www.shaffihdauda.co.tz: Umeoa? Kama ndiyo una watoto wangapi?

Abbas Pira: Sijaoa bado na sina watoto.

www.shaffihdauda.co.tz: Unaizungumziaje timu ya taifa, unafikiri wapi inakosea hadi kushindwa kusonga mbele zaidi?

Abbas Pira: Timu yetu ya taifa ime-improve sana tumepiga hatua kubwa na sifa zimuende Marcio Maximo ndiyo aliyeanzisha mfumo wa timu za vijana ambazo tunaona matunda ya soka sasa Tanzania.

Sisi tumepiga hatua kubwa Tanzania tuna uwanja mzuri tunauwezo wakuwafunga team kubwa kama Cameroon, Morocco zamani ilikuwa hatuwezi kuzifunga hizi timu nafikiri tuwape muda wachezaji na ma kocha tutasonga mbele kama kwenye mashindano ya mataifa ya Africa.

Pira akiokoa moja ya 'kash-kash' langoni mwake
Pira akiokoa moja ya 'kash-kash' langoni mwake

www.shaffihdauda.co.tz:Tofauti na mchezo wa soka, upenda kufanya kitu gani?

Abbas Pira: Baada ya soccer napenda sana boxing na napenda kuogelea.

www.shaffihdauda.co.tz: Kitu gani ambacho sijakuuliza lakini ungependa kukielezea?

Abbas Pira: Namshukuru mamangu sana yeye ndiyo alikuwa ananipa moyo kwenye kipaji changu.



Comments