Utatu hatari wa MSN – Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar – umeiangamiza Arsenal kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya Barcelona kushinda 3-1.
Kwa ushindi huo uliopatikana Nou Camp, Barcelona wanatinga hatua ya robo fainali kwa jumla ya mabao 5-1 kufuatia ushindi wa 2-0 Emirates Stadium wiki mbili zilizopita.
Safari ya matumani ya kocha Arsene Wenger kusonga mbele kwenye michuano hiyo ilianza kupata vikwazo dakika ya 18 baada ya Neymar kufunga bao la kwanza akimalizia pasi ndefu ya Luis Suarez.
Dakika ya 51, matumani ya Wenger yakafufuka baada ya Mohamed Elneny kuisawazishia Arsenal kwa mkwaju wa mbali, lakini dakika 14 baadae Luis akaifungia Barcelona bao la pili.
Msumari wa mwisho kwenye sanduku la Arsenal ukagongelewa na Lionel Messi aliyefunga bao la tatu dakika ya 88.
Barcelona XI (4-3-3): Ter Stegen, Dani Alves, Mascherano, Mathieu, Jordi Alba, Rakitic (Arda Turan 77), Busquets, Iniesta (Sergi Roberto 72), Suarez, Messi, Neymar
Arsenal XI (4-2-3-1): Ospina, Bellerin, Gariel, Koscielny, Monreal, Flamini (Coquelin 45), Elneny, Iwobi (Giroud 72), Ozil, Alexis Sanchez, Welbeck
Comments
Post a Comment