Mpango wa Real Madrid kumsajili upya Morata na kumuuza kwa faida aidha Bayern or Arsenal


Mpango wa Real Madrid kumsajili upya Morata na kumuuza kwa faida aidha Bayern or Arsenal

Real Madrid wana mpango kabambe wa kushughulikia suala la usajili wa Alvaro Morata. Lakini sio mpango ambao mashabiki wao wengi walikuwa wakiutegemea.  

 Baada kuonyesha kiwango bora akiwa na Juventus, mashabiki wengi wa RealMadrid walipiga kura kwenye mtandao wa AS na kuonyesha namna wanavyohitaji Morata arejee Santiago Bernabeu. Sasa japokuwa mpango wa kumrejesha upo lakini hili litafanyika ili waweze kumuuuza kwa faida kubwa zaidi ……….. Na tayari kuna vilabu kadhaa tayari vimeanza kufikiria kutuma ofa ya kumsajili. 

  Katika Premier League – ligi ambayo itawapa mkataba mnono vilabu vyake kutokana na dili jipya la haki za matangazo ya TV – Arsenal inaongoza mbio za kuwania saini ya Mhispaniola hiyo. Mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich ambao walisumbuliwa sana na Morata walipokutana na Juve wiki iliyopita- nao wameonyesha nia na meneja wao anayefuata, Carlo Ancelotti, ni kocha anayemhusudu sana Morata. 

Hata hivyo Morata anaripotiwa kuwaambia Madrid kama wanamhitaji basi yeye hayupo tayari kurudi kuwa mchoma mahindi kwenye benchi baada ya kuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza cha mabingwa wa Italia. Madrid na Juventus wapo kwenye mazungumzo ya kutafuta namna ya kukamilisha biashara hii, Madrid wana haki ya kimkataba ya kumnunua upya Morata kama yalivyokuwa makubaliano yao wakati Morata aliposaini mkataba wa miaka mitano. 

 Morata aliuzwa kwa 20 million euros lakini katika makubaliano kulikuwa na haki ya kumnunua katika tarehe maalum walizokubaliana 1-15 July aidha mwaka 2016 au 2017. Bei ya kumnunua upya Morata itaamuliwa kulingana na namba ya michezo atakayocheza – lakini itakuwa kati ya 20-30 million euros. Kulingana na michezo ambao Morata ameshaitumikia Juven, inategemea Madrid watalipa kiasi cha zaidi ya €25m na baada labda kumuuuza kwa kiasi cha  50 million na kutengeneza faida.   
Kwa upande we Juventus tayari wameanza kujiandaa na maisha baada ya Morata na mkurugenzi wako mkuu, Beppe Marotta, aliongea na RAI kuelezea kwamba Madrid wana haki ya kumsajili upya Morata na tayari wameanza kuangalia machaguo ya kumrithi. 



Comments