MKWASA AIFUNGUA SIRI YA USHINDI WA STARS UGENINI


MKWASA AIFUNGUA SIRI YA USHINDI WA STARS UGENINI
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Charles              Boniface Mkwasa
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Charles Boniface Mkwasa

Baada ya timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kupata ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Chad, kocha mkuu wa Stars Charles Boniface Mkwasa amesema, pamoja na hali ya hewa kuwa ngumu lakini wachezaji walicheza kwa kujituma na kufuata maelekezo na ndiyo siri ya mafanikio.

Mkwasa pia amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wa marudiano utakaochezwa siku ya Jumatatu kwenye uwanja wa taifa.

"Kwanza namshukuru Mungu kuweza kupata ushindi huu, ni ushindi mgumu na tumekuwa na presha muda wote wa mchezo na tulipoteza 'concentration' kipindi cha pili nafikiri kwasababu ya hali ya hewa lakini vijana wamejitaidi na wameweza kujituma katika hali ngumu tumecheza katika mazingira magumu sana".

"vijana wanastahili pongezi tumeweza kufanya vizuri na wameweza kutekeleza matakwa ya watanzania".

"Tulikuwa tunataka tupate magoli mapema lakini tukashindwa kupata magoli mengi mapema kwasababu ya hali ya hewa, jua lilikuwa ni kali sana wachezaji wakati wote wanakuja nje kupoza viatu ambavyo vilikuwa vinapata moto".

"Tunashukuru tumepata goli kipindi cha kwanza licha ya kupoteza nafasi nyingi lakini kipindi cha pili hatukuwa na umakini zaidi wameweza kutushambulia sana kwasababu na sisi tulikuwa tunajilinda zaidi tulikuwa tunashindwa kutoka kwenye goli letu".

"Lengo la kumtoa Mwinyi Kazimoto na kumuingiza John Bocco lilikuwa ni kusaidia kuongeza nguvu katikati na baada ya hapo tukaona pia tuongeze nguvu kwenye defense kwasababu waliamua kutumia mipira mirefu ili iwe rahisi kufika kwenye goli letu kwahiyo tukaamua kutoa mshambuliaji na kumuingia beki  kwasababu tumepata goli moja na mechi ni ugenini bora kujilinda kuliko kupoteza ushindi".

"Watanzania wawe pamoja na sisi, waje kwa wingi uwanjani waisapoti timu yao mechi itakuwa siku ya Jumatatu na sisi nadhani tunaondoka kesho kwahiyo waje kwa wingi kwasababu wingi wao utawafanya wachezaji kucheza kwa nguvu na kwa moyo zaid"i.



Comments