MARCELO HAAMINI KAMA NEYMAR ATASAJILIWA REAL MADRID



MARCELO HAAMINI KAMA NEYMAR ATASAJILIWA REAL MADRID
Brazilian sensation            Neymar has been ordered to pay £36m in back taxes, interest            and fines in Brazil
BEKI wa kushoto wa Real Madrid, Marcelo anadhani kuwa itakuwa ngumu kwa klabu yake kumsainisha staa wa Barcelona, Neymar.

Akizungumza na Globoesporte, Marcelo alieleza kuwa yeye na Neymar hawazungumzi sana kuhusu soka wakati wakiwa pamoja katika majukumu ya kimataifa na kikosi chao cha Brazil, lakini haamini kama straika huyo atajiunga naye Santiago Benabeu.

 Marcelo alipoulizwa uwezekano wa Neymar kutua Madrid alisema: "Tunafanya masihara kuhusu mambo mengine [anacheka]. Hatuzungumzi sana kuhusu soka, hivyo sijui...  Lakini nadhani itakuwa ngumu kwa Neymar, ambaye ametengeneza historia na Barcelona kuja Real Madrid. Nadhani itakuwa ngumu."

Kumekuwa na tetesi zikimuhusisha Neymar kujiunga na Madrid, ingawa staa huyo akizungumza na mtandao wa Globo ameonyesha kutokuwa na mpango wa kuondoka Nou Camp, hali inayokazia fikra za Marcelo.


"Nina furaha sana Barcelona. Ni timu ambayo najisikia nipo nyumbani," alisema Neymar na kuongeza kuwa yuko vizuri na wachezaji wenzake na kwamba haoni kama ataondoka Barcelona.


Comments