MANCHESTER UNITED YAKARIBIA KUMNASA KINDA TAHITH CHONG WA FEYENOORD



MANCHESTER UNITED YAKARIBIA KUMNASA KINDA TAHITH CHONG WA FEYENOORD

MANCHESTER UNITED inaelezwa kukaribia kukamilisha dili la uhamisho wa kinda wa Feyenoord, Tahith Chong na kuwabwaga wapinzani wake katika Premier League ambao pia wanamfukuzia staa huyo.

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 16, ambaye anamudu kucheza kama kiungo mshambuliaji, winga wa kushoto ama mshambuliaji wa kati, amekuwa akihusishwa pia na klabu kibao za Premier League zikiwamo Arsenal na Chelsea.

Hata hivyo, MailOnline imedai kuwa kinda huyo anapendelea kuhamia Old Trafford na wawakilishi wa United wanatumaini kukamilisha dili kuelekea dirisha lijalo la usajili wa kiangazi.

Chong alizaliwa katika kisiwa cha CuraƧao kilichopo kusini mwa bahari ya Caribbean katika bara la Amerika ya Kaskazini, lakini alihamia Uholanzi akiwa mtoto na akaingia katika shule ya soka ya Feyenoord tangu akiwa na miaka 10.

Tayari ameiwakilisha Uholanzi akiwa na kikosi cha vijana wa umri wa chini ya miaka 17.


Comments