Manchester United bado wanahaha kumfuatilia kinda wa maajabu Renato Sanches mwenye umri wa miaka 18 anayekipiga na klabu ya Benfica ya Ureno.
Maskauti wa United Jumanne usiku walikwenda kuangalia mechi ya Ureno na Ubelgiji ili kujiridhisha na kiwango cha mshambuliaji huyo mwenye thamani ya pauni milioni 50.
United imedhamiria kumnyakua kinda huyo katika dirisha la usajili la kiangazi ingawa bado inafanya juhudi za kuangalia uwezekano wa kushushiwa bei.
Renato Sanches, hapa akiichezea Ureno dhidhi ya Ubelgiji
Maskauti wa United walikuwepo katika mji wa Leiria Jumanne usiku kumtazama kinda huyu katika mechi ya Ureno na Ubelgiji
Comments
Post a Comment