MANCHESTER CITY YATINGA ROBO FAINALI CHAMPIONS LEAGUE LAKINI YAMPOTEZA NAHODHA VINCENT KOMPANY


MANCHESTER CITY YATINGA ROBO FAINALI CHAMPIONS LEAGUE LAKINI YAMPOTEZA NAHODHA VINCENT KOMPANY

Manchester City imetoka sare ya 0-0 na Dynamo Kiev kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Jumanne usiku ndani ya dimba la Etihad Stadium, sare inayowavusha hadi robo fainali.

City inanufaika na ushindi wao wa 3-1 ugenini, lakini pamoja na kusonga mbele kwenye michuano hiyo, klabu hiyo imepata pigo baada ya nahodha wake Vincent Kompany kuumia dakika ya 7 na kutolewa nje nafasi yake ikichukuliwa na Mangala.

Vincent Kompany ambaye amekuwa kimeo msimu huu kwa majeraha ya mara kwa mara, huenda akawa nje ya dimba kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Manchester City (4-2-3-1): Hart 7; Zabaleta 7, Kompany 6 (Mangala 7, 6), Otamendi 6 (Demichelis 24, 6.5), Clichy 7; Fernando 6, Fernandinho 6.5; Navas 6, Toure 6, Silva 6 (Sterling 79); Aguero 7

Dynamo Kiev (4-1-4-1): Shovkovskiy 6; Vida 7, Dragovic 6, Khacheridi 6, Antunes 6.5; Veloso 6; Yarmolenko 6.5, Buyalskiy 6, Garmash 6 (Sydorchuk 64, 6), Gusev 6 (Yakovenko 62, 6); Teodorczyk 6 (Gonzalez 46, 6)






Comments